TANZANIA NCHI YANGU

SMATIKA

SMATIKA

WAFADHILI

Wednesday, October 5, 2016

BIASHARA YAKO ISHINDWE NA ILEGEE


JAMAA ALIENDA KUMUONA MTUMISHI WA MUNGU WA KANISA JIPYA LILILOANZA MTAANI KWAKE. Nia kuu ilikuwa kuomba kuombewa ili biashara yake iende vizuri.
Mapunda: Mchungaji niombee
Pasta : Sema mwanangu nini tatizo? 
Mapunda : Maadui zangu wananiandama biashara yangu inaanguka mchungaji
Pasta : Hilo sio tatizo mbele ya Bwana. Piga magoti nikuombee. Biashara yako ikue. Waumini wa kanisa langu wawe wateja wao. Familia yangu itumie biashara yako, majirani zako wakutegemee
Mapunda : Amennnnnnn ooooooh Pasta asante sana
Pasta : Usinishukuru mimi mshukuru aliye juu ndie kakufungulia biashara yako mwenyewe utashangaa. Hivi unafanya biashara gani ili nitangaze wakati wa Ibada upate wateja wengi
Mapunda :Pasta kazi yangu kuchonga majeneza
Pasta: We we we, ushindwe na ulegee, biashara yako ife, familia yangu wasikuone, maadui zako wafanikiwe  kwa kila jambo ondoka upesi

No comments:

Post a Comment