TANZANIA NCHI YANGU

SMATIKA

SMATIKA

WAFADHILI

Friday, June 23, 2017

VIJANA HUENDA WAPI KUPUMZIKA BAADA YA KAZI?

Je vijana wa Tanzania huenda wapi kupumzisha akili zao baada ya kazi? Hili swali bahati mbaya sana halimo katika ajenda ya viongozi wa Tanzania, hata wale viongozi wa makundi ya vijana. Hakuna anaewaza kubuni miradi ya kutengeneza sehemu za aina hiyo, hata viwanja au majengo ambayo viongozi wa zamani waliyaweka kwa shughuli hizo 'social centers', viongozi wa sasa wanazivunja na kuporomosha majengo ambayo wao huita miradi na kusahau kabisa kuwa vijana wanastahili kuwa na maeneo ya kupumzisha akili. Ziko wapi social halls zilioachwa na akina Joseph Nyerere? Ziko wapi community centers zilizoachwa na wakoloni? Matokeo ya dhambi hii ni vijana kuishia kukutana katika kumbi za bar na vijiwe visivyo rasmi. Hahihitaji akili nyingi kujua kuwa mazoea ya kufika katika maeneo ya aina hiyo huzalisha mapenzi ya ulevi wa pombe na hatimae dawa za kulevya. Na hakika kukosekana kwa burudani mbadala huishia vijana kuona burudani nyingine pekee ni ngono. Sikiliza tungo za nyimbo na hadithi za vijana wa leo, angalia video na filamu asilimia kubwa  ni kutukuza pombe na ngono. Uvaaji na uchezaji wa mabinti ni wa kuelekeza kuwaza ngono, si ajabu kukuta moja ya biashara zinazolipa ni guest houses. Utumiaji mkubwa wa dawa za kulevya ni matokeo ya kukosekana sehemu halali za vijana kukutana kupeana mawazo bora. Tulikomboe Taifa la kesho kwa kuhakikisha si kuhamasisha viwanja vya michezo tu, pia maeneo ya shughuli nyingine za kijamii za vijana. Si kila kijana anapenda au anajua kucheza mpira, hivyo kuhamasisha kutenga  viwanja vya michezo tu hakika haitoshi.
John Kitime

No comments:

Post a Comment