Mkurugenzi wa kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa
Suhail Esmail Thakore akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake juu
ya mafanikio ya sekta ya viwanda yanavyozidi kukua na kumpongeza Rais
wa awamu ya tano Dr John Pombe Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya
kuinua sekta viwanda hapa nchini.
Mkurugenzi wa kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa
Suhail Esmail Thakore akiwa na waandishi wa habari wa mkoani Iringa wakitembelea maeneo ya kiwanda cha Ivori Iringa
Mkurugenzi wa kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa Suhail Esmail Thakore akiongea na waandishi wa habari katika jengo jipya ambalo litafunguliwa kiwanda kipya hivi karibuni
Mkurugenzi wa kampuni ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa
Suhail Esmail Thakore akiwa kwenye picha ya pamoja na waandishi wa habari wa mkoa wa Iringa pamoja na mdau wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hamza Ginga.
Na Fredy Mgunda,Iringa.
KAMPUNI
ya Iringa Food and Beverage na Ivori Ltd ya mjini Iringa imempongeza Rais Dk
John Magufuli kwa namna alivyolipatia ufumbuzi suala la sukari ya viwandani ikisema
litanusuru viwanda vilivyotaka kufungwa kutokana na uhaba wa bidhaa hiyo.
Akizungumza
na wanahabari wakati akielezea mafanikio na changamoto uzalishaji katika
viwanda hivyo, mkurugenzi wa kampuni hizo, Suhail Esmail Thakore alisema
wamepokea kwa furaha kubwa uamuzi wa serikali wa kushughulikia upungufu huo.
“Namshukuru
Mheshimiwa Rais kwa kuchukua hatua ya haraka sana kushughulikia tatizo la
sukari. Taarifa tuliyopata mara baada ya kikao kile ni kwamba taratibu za
kupata vibali vya kuagiza sukari ya viwandani kwa kuzingatia mahitaji ya
viwanda vyetu zinaendelea. Hii imetupa uhakika wa kuendelea na uzalishaji,”alisema.
Alisema
viwanda vyake viliingiwa na hofu ya kusimamisha uzalishaji baada ya serikali
kuzuia uagizaji wa sukari hiyo toka Novemba mwaka jana.
“Viwanda
vyetu vinavyo tumia malighafi zinazozalishwa na wakulima wa ndani ya nchi,
zinazalisha bidhaa mbalimbali zinazojulikana kwa jina la Ivori zikiwemo tomato
na chilli sauce, pipi, chocolate na unga wa cocoa,” alisema.
Katika
kipindi cha miaka michache iliyopita, Thakore alisema kumekuwepo na ongezeko la
matumizi ya bidhaa hizo ndani ya nchi, na zinahitajika sana katika nchi jirani
za Kenya, Kongo, Rwanda na Burundi hali inayowasukuma kuongeza uwekezaji ili
kuunga mkono azma ya Rais ya Tanzania ya Viwanda.
Thakore
alisema kwa sasa viwanda vyao vinazalisha asilimia 30 tu ya mahitaji yao yote ya
soko na katika kukabiliana na changamoto hiyo wameanza na ujenzi wa kiwanda
kipya cha pipi kitakachowawezesha kufikia hadi asilimia 50 ya soko.
“Tunatarajia
kufungua kiwanda hicho kipya kati ya mwezi Juni na Julai mwaka huu. Na mwaka
2019/2020 tutaanza ujenzi wa kiwanda kingine kikubwa cha kuzalisha bidhaa hizo
hatua itakayotuwezesha kukaribia mahitaji ya soko letu,” alisema.
Akitoa
mfano wa mahitaji ya soko la nje ya nchi, mfanyabishara huyo alisema walitakiwa
na wafanyabiashara wa Burundi kusambaza tani 30 za bidhaa hizo kila mwezi
lakini wanashidwa kufikia kiwango hicho kwa sababu uzalishaji wa sasa
hauwawezeshi kufanya hivyo.
Akizungumzia
mahitaji ya sukari kwa ajili ya viwanda vyao alisema, wanahitaji zaidi ya tani
1,600 kwa ajili ya kiwanda cha Ivori Ltd na tani zaidi ya 1,500 kwa ajili ya
kiwanda cha Iringa Food and Bevarage.
“Hata
hivyo mahitaji hayo yataongezeka mara mbili zaidi kutokana na upanuzi wa
kiwanda tunaofanya. Kwa hiyo tutaiomba serikali itusaidie kupata sukari hiyo ili
kukidhi mahitaji ya viwanda vyote na upanuzi wake,” alisema.
Thakore
alitoa wito kwa watanzania kujiwekea kipaumbele cha kutumia bidhaa za ndani ili
kuinua maendeleo ya viwanda, na kuongeza ajira na mapato ya wadau na Taifa.
No comments:
Post a Comment